Karl Heiz Rummenigge,ambaye anaongoza muungano wa vilabu vya ulaya ECA amesema kuwa kiongozi wa shirikisho hilo la soka duniani ameshtumiwa vya kutosha.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Ujerumani Magharibi pia anaamini kwamba FIFA inabadilika kwa njia nzuri.
Sepp Blater
Blatter mwenye umri wa miaka 79 anatafuta kuchaguliwa kwa mara ya tano kama rais wa FIFA.
Anapigiwa upato kuwashinda wapinzani wake watatu akiwemo Louis Figo,Michael Van Praag na Prince Ali wa Jordan katika uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo mwaka huu.
''Katika majadiliano yetu nimekuwa nikihisi kwamba yeye Blatter amesikitishwa na shutuma ambazo zimemkabili kutoka kwa vyombo vya habari'', alisema Rummenigge.