Rais Edgar Lungu alitenga siku hiyo kuwa ya kuomba msamaha na maridhiano, lengo kuu likiwa kuomba usaidizi kutoka kwa Mungu kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi
yanayokabili taifa hilo.
Raia wameombwa kutojihusisha katika shughuli za burudani na wamiliki wa mabaa wameombwa kuyafunga siku hiyo.
Shirikisho la Soka la Zambia (Faz) limeamua kuitikia wito wa rais.
"Ni wakati wetu sote kunyenyekea tena kwa Mungu, kutia nguvu uhusiano wetu naye na kumuomba kuongoza maisha yetu, mchezo wetu na taifa letu,” mkuu wa Faz Kalusha Bwalya amesema.
Mechi zilizopangiwa kuchezwa wikendi hii zitachezwa Jumatano Okotba 21, mwandishi wa BBC Kennedy Gondwe anasema.
Sarafu ya Zambia kwa jina kwacha ilishuka thamani sana mwezi Septemba huku bei ya shaba nyekundu nayo pia ikishuka pakubwa.
Taifa hilo la kusini mwa Afrika linakabiliwa na changamoto za kushuka kwa bei za bidhaa zinazouzwa nje, athari za kubadilika kwa tabia nchi na hali ngumu katika uchumi wa dunia, waziri wa fedha wa taifa hilo Alexander Chikwanda alisema akisoma bajeti ya mwaka 2016 wiki iliyopita.