come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

UTAIPENDA TU..., YANGA SASA NI MBELE KWA MBELE. YAMTANDIKA STAND UNITED 3-1

Na mwandishi wetu Shinyanga.

UTAIPENDA TU..., hivi ndivyo unavyoweza kusema kwa klabu kongwe ya mpira wa miguu hapa nchini yenye maskani yake mitaa ya twiga na jangwani, Dar es salaam Youngs African (Yanga) baada ya kuitembezea kichapo cha mabao 3-1 timu ya Stand United ya mjini Shinyanga.

Katika mchezo huo Yanga ilikuwa ya kwanza kujipatia goli la kuongoza katika dakika ya pili tu ya mchezo, mzimbabwe Donald ngoma aliweza kuwanyanyua mashabiki vitini, baada ya kuifungia goli safi la kuongoza.

Mambo yalizidi kuwawia mabaya zaidi timu ya Stand United, hasa baada ya wachezaji wa Yanga kulishambulia mfululizo lango lao, ambapo mashambulizi hayo yaliweza kusababisha madhara katika timu ya Stand, baada ya mzimbabwe Donald ngoma kwa mara nyingine tena kuiandikia timu yake goli la pili kunako dakika ya 44 kipindi cha kwanza.

Hadi kufikia mapumziko Yanga wametoka katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, wakiwa mbele kwa mabao hayo 2-0 yaliyowekwa kimiami na mzimbabwe Donald ngoma

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuendelea kulisakama lango la Stand United, na kama ilivyo kawaida ya mrundi wa Yanga Amis Tambwe, akajizubaishazubaisha uwanjani na walinzi wa Stand wakamsahau akaifungia timu yake goli la tatu kunako dakika ya 36 kipindi cha pili.

Stand United walipata goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati kupitia mchezaji wake tegemeo Elius Maguli hivyo kufanya hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika, ubao wa matangazo usomeke Stand United 1 Yanga SC 3.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa imefikisha pointi 68 ikiwa imecheza michezo 27, na sasa inahitaji pointi tatu tu ili waweze kutangazwa  "machampioni"

Wachezaji wa Yanga wakishangilia moja ya magoli waliyoshinda Kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga