Na mwandishi wetu
YANGA ya Dar es salaam leo wamezidi kujiimarisha kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Toto Africa katika uwanja wa CCM kirumba mjini Mwanza
Toto wenyewe ndio walikuwa wa kwanza kujipatia goli kupitia kwa mchezaji wao William Kimanzi kunako dakika ya 36, na goli hilo lilidumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, lakini Yanga waliweza kusawazisha goli hilo kunako dakika ya 50 kipindi cha pili kupitia mchambuliaji wake raia wa Burundi Amis Tambwe.
YANGA ilionyesha kandanda safi katika kipindi cha pili, walifanikiwa kupata goli la pili na la ushindi kupitia kwa mchezaji wake Juma Abdul kunako dakika ya 77 na kuifanya Yanga imalize mchezo huo kwa ushindi wa mabao 2-1.
Kwa ushindi wa leo, Yanga imefikisha pointi 65 nyuma ya Azam fc inayoshika nafasi ya pill, ikifuatiwa na Simba inayoshika nafasi ya tatu.