come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA YATAKATA UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINE, YAITUNGUA MBEYA CITY 2 - 0.

Na Elias John, Mbeya.

MABINGWA wa ligi kuu Tanzania Bara, Dar es salaam Youngs African leo wameendelea kutakata katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya baada ya kuwatungua wenyeji Mbeya City mabao 2-0.

Mabao ya Yanga yalifungwa katika vipindi viwili tofauti ambapo goli la kwanza lilipatikana katika kipindi cha kwanza na mfungaji akiwa beki kisiki wa timu ya Taifa ya Togo Vincent Bossou.

Katika mchezo huo Yanga ililazimika kufanya mabadiliko katika dakika ya 8 tu, baada ya mchezaji Mbuyu Twite kuchezewa rafu mbaya na mchezaji wa Mbeya City, rafu iliyosababisha Mbuyu Twite kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Salum Telela.

Kunako dakika ya 28 kipindi hicho hicho cha kwanza, Yanga ilifanya mabadiliko mengine baada ya mfungaji wa goli la kwanza la Yanga Vincent Bossou kufanyiwa rafu iliyosababisha kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Kevin Yondani.

Mashabiki waliovalia jezi za rangi ya zambarau walitaka kuondoa radha ya mchezo huo, baada ya kuanza kurusha vyupa uwanjani kunako dakika ya 44, lakini uliimalishwa na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga imetoka uwanjani ikiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya Mbeya City kulisakama lango la timu ya Yanga, lakini uhodari wa mabeki wa Yanga, ulisaidia kuliweka lango lao katika hali ya usalama.

Kunako dakika ya 36 kipindi cha pili Yanga ilifanya tena mabadiliko baada ya kumtoa Deus Kaseke na kumuingiza Stefano Mwashuya.

Mambo yalizidi kwenda mlama kwa timu ya Mbeya City, baada ya mganda Amis Tambwe kuifungia timu yake goli la pili kunako dakika ya 39 kipindi cha pili.

Hadi mwamuzi wa mchezo huo anapuliza filimbi ya mwisho, Yanga imetoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa magoli 2-0.

Amis Tambwe  akiwa na wachezaji wenzake wakishangilia goli.