Na mwandishi wetu Dundo, Angola
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC, leo wamejihakikishia kufuzu kucheza hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Taifa. Yanga waliweza kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani kwa kuitandika Sagrada Esperanca ya Angola mabao 2-0.
Katika mchezo wa leo Yanga ikiwa ugenini imekubali kufungwa goli 1-0 na Sagrada Esperanca, goli lililopatikana katika kipindi cha kwanza kunako dakika ya 25 likifungwa na mshambuliaji L. Kapungula.
Hadi kufikia mapumziko, wenyeji Sagrada Esperanca wametoka uwanjani wakiwa mbele kwa goli 1-0, goli lililofungwa na L. Kapungula.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, ambapo Yanga walijitahidi kusawazisha goli hilo na wenyeji nao walijitahidi ili waweze kuongeza goli lakini kipindi hicho cha pili milango yote ilikuwa migumu.
Kwa matokeo hayo ya mchezo wa leo Yanga kufungwa 1-0 na Sagrada, sasa yamefanya matokeo ya jumla kuwa Yanga 2 Sagrada 1, matokeo ambapo yameipaisha Yanga kucheza hatua ya robo fainali.