come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ANELKA AFUNGIWA MECHI TANO

Nicholas Anelka

Fowadi wa West Bromwich Albion Nicolas Anelka amepigwa marufuku mechi tano na kupigwa faini ya pauni 80 000 kwa kufanya ishara inayodaiwa kuwa dhidi ya Wasemiti wakati wa mechi Desemba, Shirikisho la Soka Uingereza lilisema Alhamisi.

Mfaransa huyo, aliyepiga saluti ya"quenelle" baada ya kufunga wakati wa sare ya 3-3 dhidi ya West Ham United Desemba 28, pia ameagizwa kuhudhuria na kozi ya mafunzo kwa lazima.

“Tume Huru ya Kinidhamu imempata Nicolas Anelka na hatia ya kukiuka Kanuni E3 ya FA na kumpiga marufuku ya mechi tano na faini ya pauni 80 000, akisubiriwa akate rufaa,” FA ilisema kupitia taarifa.

Adhabu hiyo haitatekelezwa hadi uamuzi kuhusu rufaa yoyote ambayo atawasilisha au hadi mchezaji huyo afahamishe FA kwamba hatakata rufaa.
West Brom, hata hivyo, tayari wamemsimamisha kucheza mara moja hadi kukamilishwa kwa shughuli ya kinidhamu ya shirikisho hilo na wamesema watafanya uchunguzi wao wa kibinafsi.


"Klabu haiwezi kupuuza madhara ambayo vitendo vyake vimesababisha, hasa kwa Wayahudi, na pia sifa za klabu,” klabu hiyo ilisema kupitia taarifa.

FA ilimpata Anelka na hatia ya kufanya ishara ambayo “ilikuwa ya kuchukiza na/au isiyofaa/au ya matusi na/au isiyokubalika.”

Adha, shirikisho hilo lilisema hilo lilikuwa “kosa la kuzidishwa” kwani lilihusisha “kurejelewa kwa asili ya kikabila na/au kirangi na/au dini au imani.”

FA iliongeza kwenye taarifa kwamba “haikumpata Nicolas Anelka kuwa mwenye chiku dhidi ya Wasemiti na wala hakunuia kuonyesha au kuendeleza chuki dhidi ya Wasemiti kwa kutumia ishara hiyo ya quenelle".
Anelka alikanusha madai kwamba yeye anachukia Wasemiti au kwamba ni mbaguzi wa rangi na badala yake akasema ishara hiyo, ambayo imeelezwa kama saluti ya Nazi iliyopinduliwa, ilikuwa ya kuonyesha heshima kwa mchekeshaji Mfaransa na ambaye pia ni rafiki Dieudonne M'Bala M'Bala ambaye aliianzisha.

West Brom walisema kwa sasa wanasubiri ufafanuzi wa uamuzi wa jopo hilo kwa njia ya maandishi, ambapo kutoka hapo Anelka ana siku saba za kuamua kama atakata rufaa.
Ishara hiyo tayari imeathiri klabu hiyo.

Zoopla, huduma ya kutafuta habari za uuzaji na ukodishaji wa nyumba na mashamba mtandaoni inayomilikiwa na mfanyabiashara Myahudi Alex Chesterman, imesema haitatia saini tena mkataba wake wa ufadhili wa jezi za West Brom wa thamani ya pauni milioni tatu baada ya msimu huu kuisha kutokana na vitendo vya Anelka.