come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SPURS WAISHANGAZA DNIPROI, PORTO, MAPOLI ZASHINDA

Emmanuel Adebayor

Emmanuel Adebayor alifunga mabao mawili katika dakika mbili na kuwezesha Tottenham Hotspur kufuta deni la mabao mawili na kushinda Dnipro Dnipropetrovsk waliokuwa wamesalia 10 uwanjani kwa mabao 3-2 kwa jumla katika Europa League, Alhamisi. Ushindi huo uliwawezesha kusonga mbele na kufika 16 bora katika dimba hilo.

Ilikuwa safari ya dhiki ya kurudi London kwa kocha wa zamani wa Tottenham Juande Ramos ambaye timu yake ilikuwa imechukua uongozi kupitia Roman Zozulya, ambaye alifukuzwa uwanjani baada ya Christian Eriksen kusawazisha na kisha mabao mawili ya Adebayor kuwezesha Spurs kusonga.

Nabil Ghilas wa Porto alifunga dakika ya 86 na kuwawezesha kupata sare ya 3-3 dhidi ya Eintracht Frankfurt, timu hiyo ya Ureno ikisonga mbele kutokana na mabao ya ugenini, nao Napoli na Ludogorets wakashinda mechi za kusisimua.


Timu hiyo Serie A ilifunga mabao mawili dakika za mwisho na kushinda Swansea City 3-1 usiku huo na kwa jumla nayo timu hiyo ya Bulgaria Ludogorets ikabandua Lazio kutokana na bao la dakika ya 88 la Juninho Quixada lililowawezesha kushinda 3-3 mechi hiyo na 4-3 kwa jumla.

Juventus walilaza Trabzonspor 2-0 kwa urahisi baada ya kushinda kwa mabao sawa Italia wiki jana nao Benfica wakafunga mabao matatu katika dakika tisa za kipindi cha pili na kulaza PAOK 3-0 usiku huo na 4-0 kwa jumla.

Salzburg, walioshinda mechi zao zote sita ngazi ya makundi, walikamilisha kichapo kikali cha 6-1 kwa jumla dhidi ya Ajax Amsterdam, kwa kushinda 3-1 nyumbani baada ya kuwakabidhi kichapo kingine wiki iliyopita.