come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MASANJA MKANDAMIZAJI AWANANGA DIAMOND NA WEMA, ADAI MAPENZI YAO KAMA WANASOMEA UDAKTARI

“Street pastor anasema.. hili swala la diamond na wema nadhani mungu amemuhurumia mmoja wapo kati ya hao wawili. kama wangekuwa watu wa kuoana wangeshaoana uchumba gani mrefu kama wanasomea udokta????

rafiki yangu nasib, kama kweli mlipendana kwa dhati hizo kasoro zinarekebishika, maana hakuna mwanadamu aliye sahihi kwani hata wewe nasib unamapungufu yako.

Na wewe dada yangu wema lazima ujue mume ndio kichwa cha nyumba kwa maelezo hayo inaonyesha haumsikilizagi mwenzio omba msamaha tenaa na tena na ukubali kubadilika.

Mi sipendi mkiwa mnaongozana wote kwenye mashow ya usiku mume kafanye kazi mke abaki home ukirudi mwili umepoa hata ujauzito unaingiaa!! sasa woote stejini mkirudi miili ya moto si mtazaa popompoo jamaniii!! nitafurahi kusikia tofauti zenu mmezimaliza kwa amani ili mashabiki wenu wasijisikie vibaya.” aliandika Masanja.

Masanja ameamua kundika hayo kufuatia hivi karibuni msanii Diamond akiwa stejini jijini Mwanza katika shoo za Fiesta aliambatana na mpenzi wake Wema ambapo Wema alipanda stejini na kuonyesha mambo yake kitendo kilichozua utata mkubwa kutoka kwa mashabiki wake.


Mashabiki wa Wema waliandika katika kurasa zao za facebook wakimlaani Diamond kwa kumfanyisha kitendo kile Wema cha kupanda jukwaani na kukata mauno, inasemekana Diamond ameamua kumwachisha Wema shughuri zake za kucheza filamu ili ampige tafu zaidi kimuziki, Masanja naye ameamua kufunguka kuhusu tukio hilo.

Chanzo SWP