|
|
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema
atasaka straika mwingine hadi kufungwa kwa soko lakini anaamini kwamba
klabu hiyo lazima isonge mbele na kukubali kuondoka kwa Luis Suarez.
Rodgers alisema Suarez, aliyewafungia magoli 31 msimu uliopita lakini akahamia Barcelona mwezi uliopita, alimtumia ujumbe mfupi kabla ya mechi waliyoshinda 2-1 nyumbani dhidi ya Southampton Jumapili, akitakia timu hiyo ushindi.
Lakini raia huyo wa Ireland Kaskazini anaamini kuuzwa kwa Suarez, kwa takriban €81 milioni, hakutaandama klabu hiyo msimu huu.
“Ndoto yetu hapa Liverpool lazima iwe kubwa kushinda mchezaji mmoja. Klabu kubwa hupoteza wachezaji na ndoto zetu ni kubwa kushinda Luis,” akasema Rodgers baada ya mabao ya Raheem Sterling na Daniel Sturridge kuwezesha timu hiyo kuanza msimu kwa ushindi.
“Alinitumia arafa nzuri sana asubuhi akitutakia kila la kheri, ambayo ni ishara nzuri. Lakini sasa yeye ni rafiki wa Liverpool.
“Ni kijana mzuri, lakini ameenda. Moyo wake uko na Liverpool, atabaki kuwa Liverpool na ilikuwa hatua nzuri.
“Lakini tunaangalia mbele, sisi ni wakubwa kushinda mchezaji mmoja,” akaongeza.
Rodgers, ambaye amehusishwa na mastraika kadha tangu auze Suarez, alielezea hamu yake ya kuongeza fowadi mwingine kikosini.
“Bado nafikiria tunahitaji straika mwingine. Ni jambo ambalo tutaangazia lakini inategemea kama atapatikana.
“Kwa hivyo tutamtafuta hadi kufungwa kwa soko lakini mnawaona wachezaji tulio nao, ustadi tulio nao,” akasema.
Rodgers alianza na Sturridge na Sterling safu ya mashambulizi, na mchezaji mpya, fowadi wa Uingereza Rickie Lambert, akiwa kwenye benchi dhidi ya timu yake ya awali.
Meneja huyo wa Liverpool alimmwagia sifa Sturridge, aliyefunga mabao 21 ligini msimu uliopita na aliyefangia bao la ushindi dakika ya 79.
“Ninafikiri kwa Daniel kulikuwa kuendeleza tu, hayo ni mabao 36 sasa katika mechi 50 aliyofungia Liverpool ambayo nadhani ni rekodi.
“Wakati mwingine atanyamaza katika mechi lakini bado atakaa kama atafunga bao na nilifurahishwa na bao la aina hiyo, lilikuwa la kuwinda eneo la hatari, ambapo unatarajia afeli na alilielekeza kwa njia maridadi sana hadi kwenye kona ya wavu,” akasema.