|
|
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alisema anatumai
kipa Petr Cech atasalia katika klabu hiyo licha ya kupoteza nafasi yake
ya kuanza mechi kwa Mbelgiji Thibaut Courtois.
Courtois, 22, aliyerudi Chelsea baada ya kufana akiwa Atletico Madrid kwa mkopo, alitumiwa na Mourinho mechi ya kwanza ya Ligi ya Premia Jumatatu, waliyoshinda 3-1 ugenini Burnley.
Cech amekuwa kipa nambari wani wa Chelsea tangu ajiunge na klabu hiyo miaka 10 iliyopita, na alikuwa kwenye vikosi vilivyoshinda Ligi ya Premia mara tatu na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2012.
Alipoulizwa ikiwa Courtois sasa ndiye nambari moja wake kwa sehemu iliyosalia ya msimu, Mourinho alisema hataki kuangalia mbele sana.
“Sipendi tamko hilo la ‘kipindi kilichosalia cha msimu’. Yeye si wangu wa kuanza mechi kwa kipindi kilichosalia cha msimu. Alikuwa wangu wa kuanza leo na nafikiri alicheza vyema vya kutosha kuweza kuwa wangu wa kuanza mechi ijayo,” Mourinho aliambia wanahabari.
Bosi huyo wa Chelsea alisema Courtois atahitajika kusalia na mchezo wa hali ya juu kuendelea kuhifadhi nafasi yake kutokana na ushindani anaokabiliwa nao.
"Ukiwa na mchezaji stadi kando yako kama vile Petr na anayetia bidii, ukikosa kucheza vyema umo hatarini. Simo hatarini, niko salama. Chelsea haimo hatarini, Chelsea iko salama, wote ni magolikipa wazuri,” akaongeza.
Mourinho alisema anatarajia kwamba Cech atachukulia hilo kwa njia ifaayo.
"Ninataka kuweka (Petr). Klabu inataka kukaa naye na natumai anasalia,” akasema.
"Nimemjua Petr kwa miaka 10, ninajua hatalala, hataketi na kusema “Sina nafasi’, ninadhani atakuwa kinyume kabisa.
“Namtarajia afike uwanja wa amzoezi Jumatano na kuwa mtaalamu na kupigania nafasi yake tena langoni,” akaongeza.