come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA YAWA GUMZO PEMBA, KILA KONA YANGA

Na Fikiri Salum, Pemba

UMAARUFU wa klabu ya Yanga unazidi kuongezeka na sasa imeanza kuzungumzwa kila kona mjini Pemba ambapo iliwasili jana tayari kuanza ziara ya mafunzo kwa ajili ya kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho mwakani.

Kwa mujibu wa mleta habari wetu aliyepo Pemba amesema Yanga imepata mapokezi makubwa jana na mashabiki wake wanaoishi Pemba, pia mashabiki hao na wengineo wamezidi kumshangaa kocha wa timu hiyo Mbrazil Marcio Maximo ambaye ameambatana na timu hiyo.


Aidha kutua kwa Yanga Pemba kumesababisha mashabiki wengine wanaokaa Unguja nao kuifuata Yanga, mashabiki hao wamezidi kumiminika Pemba kwa madai wanataka kuwaona Yanga ambayo inasifika kwa soka zuri na la kuvutia, pia shauku ya mashabiki hao ni kutaka kuwaona kwa macho yao mastaa waliopo Yanga.

Gumzo kubwa katika kikosi cha Yanga ni kocha Maximo, Cautinho na Jaja ambao nao ni Wabrazil kama ilivyo kwa Leonaldo Neiva kocha msaidizi wa kikosi hicho, pia mashabiki wanataka kupiga nao picha mastaa wote walioambatana na Yanga.

Kitu kingine katika msafara huo wa Yanga, mashabiki wanazidi kujitokeza kumshuhudia Mrisho Ngasa, Hamisi Kiiza, Jerry Tegete na Mzanzibar mwenzao Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye yumo katika kikosi cha Yanga kwa mafanikio makubwa kuliko kwa Wazanzibar wengine wanaocheza bara.

 Wachezaji waliondoka kuelekea Pemba ni:

Walinda Mlango:

Juma Kaseja, Ally Musatfa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida"
Walinzi wa Pembeni:
Juma Abdul, Salum Telea, Oscar Joshua, Edwad Charles na Amos Abel
Walinzi wa Kati:


Kelvin Yondani, Nadir Haroub "Cannavaro", Rajab Zahir na Pato Ngonyani.
Viungo:
Mbuyu Twite, Said Juma "Makapu", Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hamis Thabit.
Viungo wa Pembeni:
Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Nizar Khalfani na Andrey Coutinho.

Washambuliaji:

Geilson Santos "Jaja", Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Hamis Kizza na Hussein Javu
Benchi la Ufundi walioko Kisiwani Pemba ni:
Kocha Mkuu: Marcio Maximo
Kocha wasaidizi Leonado Neiva, Salvatory Edward
Kocha wa Makipa: Juma Pondamali
Daktari wa timu: Dr Suphian Juma
Meneja wa timu: Hafidh Saleh
Mchua Misuli: Jaco Onyango
Mtunza Vifaa: Mahmod Omar "Mpogolo"