Kwa mujibu wa taarifa ya kifo chake iliyotangazwa mapema leo inasema kwamba marehemu Mgeni alifariki katika hospitali ya Mnazi Mmoja alikokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu, Mgeni ambaye amejipatia umaarufu kupitia muzki wa taarabu amefariki akiwa ndio kwanza ameanza kupata mafanikio.
Tasnia ya taarabu imepatwa na pigo kubwa kufuatia kifo chake hasa ukizingatia marehemu alikuwa akipigana kuufikisha muziki huo kwenye mafaniko ya hali ya juu, Wadau mbalimbali wa taarabu wamemwelezea marehemu Mgeni kwamba alikuwa msanii mahiri