Inasemekana kupigwa mawe kwa wachezaji na viongozi wa Yanga jijini Mbeya walipocheza na Mbeya City na kutoka sare ya kufungana 1-1, Wallace Karia ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ligi anahusika na mpango mzima wa sakata hilo hivyo wamepanga kumshukia.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari hizi ambacho ni rafiki wa karibu na kundi moja la wanachama wa Yanga kimedai Wanayanga wanaumizwa sana na maneno ya jeuri yanayosemwa na Karia huku akionyesha ana machungu na Yanga.
'Karia amekuwa akiikandamiza sana Yanga tangia sakata la Azam Media ambapo ameonyesha kuidharau na kuikebehi sana klabu yetu ya Yanga' kilisema chanzo hicho, Uongozi wa Yanga umekata rufaa yake jana kutaka mchezo wake na Mbeya City urudiwe kufuatia kupigwa mawe na mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Mbeya City