Akisoma Hukumu ya kesi hii Mheshimiwa Hakimu Mwakasenga alisema mlalamikaji na shahidi walipishana kwa utetezi huku mlalamikaji Danieli Simbi akisema ni shilingi Milioni mbili laki moja na kumi na tano na mia tano (2,115,5000 ) alizomkabidhi Batarokota na shahidi nae alisema ni shilingi milioni mbili na laki moja tu (2,100,000 )ndio alizokabidhiwa tena bila maandishi.
Akisoma hukumu hiyo Mheshimiwa Masenga alimwachia huru msanii Batarokota kwa kuwa ana kosa lolote na maelezo ya mashahidi na mlalamikaji ayajakidhi matakwa ya kumtia hatiani msanii Batarokota.
Msanii Batarokota amekaa Keko miezi minne toka tarehe 10/5/2013 mpaka tarehe 16/09/2013 kwa kukosa dhamani. pia Batarokota amewalaumu sana wasanii wenziwe kwa kutompa ushirikiano tangu awe mahabusu ya gereza la Keko mpaka aliposhinda kesi hapo jana