Baadhi ya mashabiki wa soka hasa wa Yanga wameelezea kwa masikitiko yao kukosekana kwa wachezaji Hamisi Kiiza, Mrisho Ngasa na Saimon Msuva kunaweza kuigharimu Yanga pindi inaposhuka uwanjani katika mechi zake muhimu za ligi kuu bara.
Wakizungumza kwa vipindi tofauti mashabiki hao wamesema kuwa Yanga ina kikosi bora lakini Kiiza, Ngasa na Msuva ndio tegemeo katika kikosi hicho na kukosekana kwao kumeigharimu timu katika mechi mbili za mwanzo.
Msuva ambaye amepewa red kadi dhidi ya Coastal Union mchango wake umeonekana katika mechi ya Mbeya City ambapo kama angekuwepo vijana hao wa Mbeya wangeiona shughuri yake, pia kukosekana kwa mfumani nyavu mahiri Hamisi Kiiza ni pengo lingine.
Mrisho Ngasa ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea Simba amejikuta amesimamishwa mechi sita na TFF kwa madai ya kusajili timu mbili, mchango wa Ngasa ndani ya Yanga ni muhimu na sasa Yanga imeingia majaribuni.