come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

STRAIKA YANGA AIPA ZAWADI YA NG'OMBE MTAMBANI FC

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Julius Mrope (Pichani) jana aliiwezesha timu ya Mtambani FC ya Tabata kutwaa zawadi ya ng'ombe mnyama baada ya kuifunga timu ya Sun Bust pia ya Tabata kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Tabata.


Katika mchezo huo wa kuvutia timu ya Sun Bst iliutawala mchezo huo katika kipindi cha kwanza lakini uimara wa mabeki wa Mtambani wakiongozwa na Kessy Mapande ulisaidia kuondoa hatari zote, Mtambani iliyochezesha nyota mbalimbali akiwemo Jabu Jabu aliyepata kuichezea Simba na Patrick Mrope wa Srengeti Boys waliweza kuwamudu Sun Bust waliokuwa na Godfrey Taita na Jma Seif 'Kijiko'.

Lakini pasi nzuri ya Juma Jabu ilimkuta Julius Mrope na kumalizia kwa shuti kali lililomuacha hoi kipa Amani Simba wa Sun Bust, Mtambani walikabidhiwa zawadi yao ya ng'ombe na mgeni wa heshima ambaye ni mjumbe wa NEC taifa