come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA KUMALIZA ZIARA KWA WAAZERBAJAIN.

Na Baraka Kizuguto, Antalya

TIMU ya Yanga SC ya Dar es Salaam leo Saa 8:00 mchana kwa saa za Uturuki sawa na saa 9:00 Alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbajain katika viwanja vya Side Manavgat.

Kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema watautumia mchezo huo kama sehemu ya mwisho ya maandalizi ya kujianda na Ligi Kuu ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo ambapo watoto wa Jangwani watafugua dimba dhidi ya Ashanti United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Mchezo wa leo utakua mgumu pia, kwani timu ya Simurq PIK ina wachezaji wazuri ambao wanatoka sehemu mbali mbali duniani na ipo katika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu nchini kwao, hivyo nadhani kitakua kipimo kizuri cha mwisho kabla ya kurejea nchini Tanzania,”alisema babu huyo.


Akiongelea kikosi chake mara baada ya mazoezi ya asubuhi, Hans amesema anashukuru mungu maendeleo ya timu ni mazuri, mabadiliko yapo na wachezaji wanaonekana kumuelewa hivyo anaamini kadri siku zinavyokwenda timu itakua katika kiwango kizuri zaidi.

“Nimeshashuhudia michezo miwili mmoja tukishinda 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK Lidi Daraja la pili Uturuki na juzi tukitoka sare ya 0-0 dhidi ya timu ya KS Flumartari ya Ligi Kuu Albania, kwa kweli nawapongeza vijana wanaonyesha kweli wanajua wajibu wao na kucheza kwa kufuata maelekezo ya walimu" alisema Hans.

Aidha, Hans amesema ni jambo jema timu imecheza jumla ya michezo mitatu, ikishinda miwili na kutoka sare mchezo mmoja, huku ikifunga mabao 5 na kutokuruhusu nyavu zake kutikisika hii yote inayonyesha timu imeiva tayari kwa mashindano yanayotukabili.

Hadi sasa hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kufuatia kiungo Hassan Dilunga kupona malaria na kuungana na wenzake katika mazoezi.