|
|
Chile walibandua mabingwa watetezi wa Copa
America Uruguay kutoka kwenye dimba hilo kwa ushindi wa 1-0 kwenye
robofainali ya kasi iliyoisha kwa utata Jumatano na kuweka hai matumaini
na taifa hilo mwenyeji kujishindia taji hilo mara ya kwanza.
Uruguay walisalia wachezaji tisa mechi ikimalizika Edinson Cavani akifukuzwa uwanjani kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya dakika 62 uwanjani naye Jorge Fucile pia akaonyeshwa kadi nyekundu kwa kuadhibiwa mara ya pili zikiwa zimesalia dakika mbili za kucheza.
Baada ya kuondoka kwa Fucile, mechi hiyo ilisitishwa kwa dakika kadha wachezaji wa Uruguay wakimzingira refa na maafisa wasimamizi wa mechi na wachezaji wa timu zote mbili walishikana mashati uwanjani.
Mabingwa hao watetezi walionekana kuonewa baada ya ushahidi wa video kuonyesha ni Gonzalo Jara aliyemzaba kofi ‘la kirafiki’ Cavani na kisha kumsukuma kutoka nyuma, jambo ambalo halikuonekana na refa.
Cavani alipogusa uso wa Jara kidogo tu, mchezaji huyo alijiangusha na kupelekea straika huyo wa Paris Saint Germain kupewa kadi ya pili ya manjano.
“Tuna uchungu mwingi sana,” meneja wa Uruguay Oscar Tabarez aliambia wanahabari. “Nimetazama televisheni na picha, huko ndiko ukweli uko.”
Mauricio Isla alifunga bao pekee la mechi hiyo dakika ya 82 alipotuma kombora wavuni akwia hatua 15 kutoka kwenye goli baada ya kipa wa Uruguaya Fernando Muslera kukosa kuondoa vyema krosi.
Wenyeji Chile, waliotawala mechi hiyo kwa kudhibiti mpira asilimia 80, hawajawahi kushinda Copa America tangu kuanzishwa kwake 1916 na watakutana na mshindi wa robofainali kati ya Peru-Bolivia kwenye nusufainali.
"Sasa tuna mechi nyingine na sijui kama itakuwa dhidi ya Peru au Bolivia lakini bado ndoto yetu iko hai,” alisema straika Alexis Sanchez.
"Tulipambana sana na nashukuru mashabiki waliotuunga mkono wakati wote.”
Kwenye robofainali hizo nyingine, Argentina watakutana na Colombia Ijumaa nao Brazil wakutane na Paraguay Jumamosi.