come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Eto’o akubali kujiunga na Antalyaspor

Samuel Etoo 

Aliyekuwa Mchezaji Bora wa Mwaka Afrika Samuel Eto'o amekubali kuhamia klabu ya Antalyaspor iliyopandishwa daraja majuzi kucheza Ligi Kuu ya Uturuki.

Klabu hiyo ilithibitisha kwamba imeingia kwenye makubaliano na Eto’o lakini mkataba bado haujatiwa saini.

Kikwazo pekee kwa sasa ni haki za picha za Eto’o nchini Italia tatizo ambalo bado halijatatuliwa.

“Tuna makubaliano na mchezaji huyo. Lakini bado kuna matatizo kuhusu haki za picha za mchezaji huyo Italia. Tutatatua matatizo hayo haraka iwezekanavyo,” klabu hiyo ya uturuki ilisema.


Tayari gazeti la Italia la Gazzetta dello Sport liliripoti kwamba rais wa Sampdoria Massimo Ferrro anaamini mchezaji huyo wa miaka 34 kutoka Cameroon amo njiani kuondoka miezi sita tu baada ya kutua Uturuki.

Ferrero alitaja kuondoka kwa Eto'o kuwa kwa mwanamume anayetaka "kufuata moyo wake na pochi lake.”
Mchezaji huyo wa zamani wa Cameroon amefana sana katika uchezaji wake akichezea FC Barcelona, Inter Milan, Chelsea na Everton.

Eto'o alishinda mataji mawili ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika, moja la Serie A, matatu ya La Liga Uhispania, dhahabu Olimpiki na vikombe vitatu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Straika huyo alitua Sampdoria Januari lakini amefunga mabao mawili tu mechi 18 alizochezea Blucerchiati.