come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

JUMA KASEJA ASHIKILIA MKATABA WA IVO MAPUNDA SIMBA.

Sintofahamu ya mlinda mlango wa Simba Ivo Mapunda juu ya kuongeza mkataba mpya kufuatia ule wa kwanza kumalizika umeshikiliwa na kipa mwenzake Juma Kaseja ambaye kwa sasa yuko huru.

Mapunda amemaliza mkataba na Simba na mpaka jana alikuwa bado ajaongezewa mwingine na bado aliendelea kusalia jijini Mbeya wakati wenzake wameanza kujifua chini ya kocha mpya Dylan Kerr.


Uwezekano wa kipa huyo kumwaga wino Simba upo mikononi mwa kipa Juma Kaseja ambaye anatajwa kurejea tena msimbazi na kwa sasa anajifua nchini Oman ili kujiweka fiti.

Kaseja alivunja mkataba wake na Yanga baada ya kujikuta akiozea benchi huku makipa wenzake Ally Mustafa 'Barthez' na Deogratus Munishi 'Dida' wakibadilishana namba