Uchumi wa Uchina umeimamarika kwa asilimia 6.9 katika robo ya tatu ya mwaka huu.
Hicho ni kwango cha chini sana tangu mwaka 2009, ingawa ni bora zaidi kuliko wachanganuzi walivyobashiri.
Kudorora kwa uchumi wa Uchina si jambo la kushangaza hivi sasa kwa kuwa mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayotokea nchini humo ni lazima yangetokea kwa sababu ya kasi
ya kukua kwa miaka kadhaa.
Lakini swali kwa sasa ni; kasi ya uchumi huo itaendelea kudorora kwa muda gani? Swali hili haliwahangaishi wafanyakazi wa viwanda pekee, katika hali ambapo tayari wafanyakazi katika viwanda wameanza kuhangaika.
Kukua kwa uchumi kwa asilimia 6.9 ni kubaya sana ikilinganishwa na miaka sita iliyopita lakini si mbaya zaidi kama walivyobashiri wachanganuzi wa kiuchumi.
Inaonekana wazi kuwa hatua iliyochukuliwa na Serikali ya kuchochea uchumi, kukiwemo kupunguza viwango vya riba kwa asilimia tano imeanza kufanya kazi kwa kiwango fulani.