Na Fikiri Salum
Wengi wanamfahamu kwa jina la Asiatu Dammbaya 'Full Mapozi' lakini mwenyewe amejitambulisha anaitwa Asia, ni mwanasalamu wa kwanza kabisa kutungiwa wimbo wa taarabu.
Asia amekuwa mdau mkubwa kwenye muziki huo hasa anapokuwepo katika vipindi vyake vya salamu, Tarehe 15 Oktoba mwanasalamu huyo aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa, Asia alizaliwa mwaka 1980.
Chakushangaza Asia licha ya kuwa mpenzi mkubwa wa muziki wa taarabu, amekuwa akipenda soka kuliko muziki huo.
Mwanasalamu anayetikisa kwa sasa kutokana na sauti yake nyororo inayoweza kumtoa nyoka pangoni ni shabiki mkubwa wa Yanga SC na amekuwa akimpenda zaidi nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Pia ni shabiki wa kupindukia wa Arsenal ya Uingereza, Asia anavutiwa na soka ya Lionel Messi wa FC Barcelona ya Hispania, akielezea salamu, Asia ambaye ni mhudumu wa afya ya binadamu (Nesi) anayemiliki duka lake la madawa (Phamacy) lililopo Temeke jijini Dar es Salaam amedai salamu ni upendo na si uadui