come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

#YANGA BWANA! NOMA SANA...

Na Elias John, Dar es salaam

MABINGWA wa ligi kuu ya VodaCom Tanzania Bara Yanga SC leo wamei tembezea kichapo timu ya Mwadui kutoka Shinyanga baada ya kuitandika mabao 2-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ilikuwa ya kwanza kupata goli kwani kunako dakika ya Tatu tu ya mchezo mchezaji Saimon Msuva aliipatia timu yake goli la kuongoza.

Goli hilo la Yanga halikudumu kipindi kirefu kwani muda mfupi tu baadae Mwadui waliweza kusawazisha goli hilo kupitia kwa mchezaji wake Kelvin Sabati.

Kipindi cha pili kilivyoanza timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu lakini juhudi za mchezaji Haruna Niyonzima zilimwezesha kuipatia timu yake goli la ushindi kunako dakika ya 86 ya mchezo.

Yanga sasa imefikisha pointi 56 nyuma ya klabu ya Simba iinayoshikilia msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 57.