Mwanadada wa
Washindani 20 walishiriki mashindano hayo kuonyesha mitindo ya kiisilamu pamoja na maadili ya kiisilamu wakati wa mashindano hayo.
Mashindano yalifanyika kabla ya shindano kubwa zaidi la mwanamke mrembo zaidi duniani, ambalo limeghadhabisha makundi ya watu wenye msimamo mkali nchini Indonesaia kwa kutaka kuandaliwa huko.
Waliofuzu kwa fainali ya mashindano hayo, walichaguliwa kutoka miongoni mwa watu 500 waliochaguliwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Moja ya vikwazo vya kuruhusiwa kushirki kwenye mashindano ilikuwa kusimulia kisa chako na ambavyo ulianza kuvalia Hijab au mtandio, ambacho kilikuwa kikwazo kwa wote waliotaka kushiriki.
Washiriki walitoka Bangladesh, Iran, Malaysia, Nigeria na Brunei.
Kabla ya fainali, washindani walihitajika kuamuka kwa sala ya asubuhi na kuswali pamoja huku wakijifunza kusoma Koran.
Bi Ajibola, mwenye umri wa miaka 21, alilia na kusoma aya kutoka kwa Korani, jina lake lilipotajwa. Alituzwa dola 2,200, pamoja na ziara ya mji mtukufu wa Mecca na nchini India.
Kabla ya kushinda alisema kuwa nia yake ya kushiriki mashindano hayo ilikuwa tu kuonyesha dunia nzima kuwa dini ya kiisilamu ni nzuri sana.
Eka Shanti, aliyefutwa kazi kwenye televisheni kwa kukataa kuvua mtandio wake, ndiye alianzisha shindano hilo miaka mitatu iliyopita.
Aliambia shirika la habari la Agence France-Presse kuwa walifanya shindano hili siku chache kabla ya shindano la kimataifa la mwanamke mrembo zaidi duniani kuonyesha wasichana kuwa kuna njia zengine tofauti ambazo unaweza kuwa mrembo.
Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa ya waisilamu duniani.