come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

WOODS AKAMIA KITITA CHA DOLA MILIONI 6.3

Tiger Woods
Tiger Woods anatarajia kushinda taji lake la sita mwishoni mwa mwaka na kujishindia dola milioni sita nukta tatu katika mashindano ya Tour yanayoanza Alhamisi.

Bingwa huyo wa dunia ni mmoja wa wachezaji watano wanaojua kuwa ushindi katika mashindano hayo mjini Atlanta yatawapa nafasi ya kujishindia kombe la FedEx Cup kwa msimu wote, wakati wachezaji watakaosali wanaweza pia kujipatia kitita cha ziada.
''Ushindi wangu mara tano mwaka huu, umekuwa jambo nzuri kwangu,'' alisema Woods.
"kama wachezaji wenzangu wanne walio katika nafasi za kwanza tano, tunajitahidi kujitengezea mustakabali wetu.''
Aliongeza kusema kuwa: '' nadhani nimecheza vyema sana. Nimeshinda mara mbili na nimemaliza wa pili mara nne. Hiyo sio vibaya katika maisaha yangu kama mchezaji wa Golf.''
Henrik Stenson, Adam Scott, Zach Johnson na Matt Kucharni wachezaji wengine wanaojua kuwa ushindi utawaweka katika nafasi nzuri kuwawezesha kupata kitita hicho wakati Woods anaweza kumaliza katika nafasi ya 29 na bado aweze kuwa katika nafasi ya kushinda.
Kwa bingwa wa mashindano ya Open Phil Mickelson kuweza kushinda , anahitaji kushinda mashindano haya ambayo yenyewe yana zawadi ya dola milioni 1.4.
Bingwa wa Uingereza Justin Rose anahitaji kuwa katika hali sawa na hiyo.