KOCHA Mholanzi wa Yanga SC, Ernie Brandts juzi ameiongoza Yanga SC kufikisha mechi 25 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara bila kufungwa hata moja tangu msimu uliopita.
Kwa ujumla, katika mechi 27 ambazo Yanga imeongozwa na beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, imepoteza moja tu mbele ya Kagera Sugar ya Bukoba msimu uliopita.
Tangu kufungwa 1-0 na Kagera, matokeo ya mechi zilizofuata ni sare na ushindi hadi Yanga kutwaa ubingwa na sasa akiwa katika kampeni za kutetea taji, amemudu kucheza mechi nne bila kufungwa, zikiwemo mbili za ugenini.
REKODI YA ERNIE BRANDTS YANGA
1. Yanga 1-1 Simba SC (Ligi Kuu)
2. Yanga 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
3. Yanga 3-1 Toto African (Ligi Kuu)
4. Yanga 3-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
5. Yanga 3-0 Polisi Moro (Ligi Kuu)
6. Yanga 1-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
7. Yanga 3-0 JKT Mgambo (Ligi Kuu)
8. Yanga 2-0 Azam FC (Ligi Kuu)
9. Yanga 2-0 Coastal (Ligi Kuu)
10. Yanga SC 3-1 Prisons (Ligi Kuu)
11. Yanga 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
12. Yanga 4-0 African Lyon (Ligi Kuu)
13. Yanga SC 1-0 Azam FC (Ligi Kuu)
14. Yanga SC 1-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
15. Yanga SC 1-0 Toto Africans (Ligi Kuu)
16. Yanga 1-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
17. Yanga SC 0-0 Polisi (Ligi Kuu)
18. Yanga SC 3-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
19. Yanga SC 1-1 JKT Mgambo (Ligi Kuu)
20. Yanga SC 3-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu) alikuwa mgonjwa hakuja Taifa.
21. Yanga SC 1-1 Coastal Union (Ligi Kuu)
22. Yanga SC 2-0 Simba SC (Ligi Kuu)
23. Yanga SC 1-0 Azam (Ngao)
24. Yanga 5-1 Ashanti (Ligi Kuu)
25. Yanga SC 1-1 Coastal U (Ligi Kuu)
26. Yanga SC 1-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
27. Yanga SC 1-1 Prisons (Ligi Kuu)
Mara baada ya kuajiriwa Yanga Septemba mwaka jana kurithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ulikuwa dhidi ya mahasimu, Simba SC ambao alitoa sare ya 1-1, kabla ya kwenda kuchapwa 1-0 na Kagera Sugar Bukoba.
Kutoka hapo, Yanga haijafungwa tena katika Ligi Kuu hadi leo, ikizifunga 3-1 Toto African, 3-2 Ruvu Shooting, 3-0 Polisi Morogoro, 1-0 JKT Oljoro, 3-0 JKT Mgambo, 2-0 Azam FC, 2-0 Coastal Union, 3-1 Prisons, 4-0 African Lyon, 1-0 Azam FC, 1-0 Kagera Sugar, 1-0 Toto Africans, 1-0 Ruvu Shooting, 3-0 JKT Oljoro, 3-0 JKT Ruvu, 2-0 Simba SC, 1-0 Azam katika Ngao ya Jamii na 5-1 Ashanti United.
Mechi nyingine imetoa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, 0-0 na Polisi Morogoro, 1-1 na JKT Mgambo, 1-1 na Coastal Union mara mbili msimu uliopita na msimu huu, 1-1 na Mbeya City na 1-1 na Prisons.
Jumapili, Brandts ataiongoza Yanga SC katika mchezo wa 27 wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, je ataendeleza rekodi ya kutofungwa? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.