come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA YAHAMISHIA HASIRA ZAKE KWA AZAM JUMAPILI

Yanga imetamba kuwa inarudi Dar es Salaam kwenye kapeti na sasa mashabiki wake wasubiri raha tu na heshima wataanza kuirudisha mechi yao ijayo na Azam FC kwa sababu walizocheza Mbeya zilikuwa na changamoto nyingi kwao.


Ingawa imekiri kuwa mechi yao na Prisons wachezaji wao walikosa umakini wakaruhusu bao la kusawazisha.

Yanga itacheza na Azam FC Jumapili baada ya kumaliza mechi zao za Mbeya walizotoka sare ya 1-1 na Mbeya City na sare ya 1-1 na Prisons ya Mbeya.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Minziro alisema kuwa, baada ya wakati mgumu waliokutana nao katika mechi hizo sasa wanarudi kwao.

“Tunarudi nyumbani kwenye kapeti sasa, heshima itarudi tu kuanzia mechi yetu na Azam,” alisema Minziro.

“Azam ni timu ngumu lakini imani yangu tutashinda. Unajua mechi za mkoani zina changamoto nyingi sana kama ulivyoona  mwenyewe,” alisema Minziro ambaye pamoja na mkuu wake, Ernest Brandts walilalamikia ubovu wa uwanja na hali ya hewa.

Akizungumzia sare na Prisons, Minziro alisema: “Tatizo lilikuwa kwenye umakini, wachezaji kwa nafasi zote hawakuwa makini, ndivyo ilivyokuwa.”

 Yanga kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 6, watani wao wa jadi, Simba wanaongoza ligi kwa pointi 10, wanafuatiwa na Ruvu Shooting na JKT Ruvu ni ya tatu.