Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ana uhakika kiungo Santi Cazorla ameiva kikamilifu baada ya kufunga mabao yake ya kwanza katika ligi ya Premier ndani ya miezi miwili.
Mabao mawili kutoka raia huyo wa Uhispania yaliihifadhi uongozi wa Arsenal katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Fulham, Jumamosi.
Cazorla alikosa wiki sita mwanzo wa musimu baada ya kujeruhi kifundo cha mguu katika mechi yao na Tottenham Hotspur mnamo Septemba 1.
“Alikosa kwa muda mrefu mwanzo wa musimu na matitizo ya jeraha. Amerejea hali yake ya umaahiri tangu Desemba kati,” Wenger alisema.
“Yeye ni mmoja wa wachezaji wanao uwezo wa kubuni kitu specheli katika ngome ya wapinzani, iwe ni kupitia pasi au kumaliza nafasi. Ana uwezo wa kucheza na miguu yote miwili na hilo linamfanya awe tisho,” aliongeza.
Cazorla aliunganisha maridadi na wenzake Jack Wilshere na Olivier Giroud kupatia Arsenal uongozi dakika ya 57 kabla ya kuongezea la pili dakika tano baadaye.
"Wilshere ananoa makali hivi sasa na amehusika katika mwanzo wa harakati zetu kwa kuongeza kasi katika mchezo wetu,” Wenger aliongeza.
Ingawa meneja huyo anadhamiria kuimarisha kikosi, alieleza kurithika kwake na maendeleo ya timu hiyo.