come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

T-SHIRTS ZINAUZWA, WADAU CHANGAMKIENI FURSA.

Na Sadallah Jabir.

WADAU wa masuala ya mavazi a.k.a kupendeza, wameshauriwa kuchangamkia fursa ya kununua T-shirts zenye ujumbe usemao USI4C NIKUAMINI kwani zina ubora na hadhi ya hali ya juu utakaokufanya uwe huru katika sehemu yoyote.

Hayo yamesemwa leo na mdau mkuu wa masuala ya mavazi hapa nchini Sadallah Jabir, alipokuwa akipiga story mbili tatu na mwandishi wa STAA WA LEO ofisini kwake maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Sadallah au kama ambavyo wengi wanapenda kumuita Saddy, amesema "USI4C NIKUAMINI" ni ujumbe unaoweza kuvaliwa na watu wa rika zote, jinsia ya aina yoyote na pia unaweza kuivaa katika sehemu yoyote bila ya kutafsirika kuwa wewe ni mtu wa aina gani.

Aidha Saddy ameongeza kuwa "USI4C NIKUAMINI ni ujumbe unaowaasa watu wote wenye tabia ya kulazimisha kuaminiwa wakati sifa za namna hiyo hawana.

Saddy ameongeza kuwa T-shirts za USI4C   NIKUAMINI zinapatikana kwenye maduka ya nguo, na kwamba mawakala waaminifu wanahitajika. Kwa maelezo zaidi piga namba 0755673743

YANGA YAPAA HADI ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

Na mwandishi wetu Dundo, Angola

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC, leo wamejihakikishia kufuzu kucheza hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Taifa. Yanga waliweza kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani kwa kuitandika Sagrada Esperanca ya Angola mabao 2-0.

Katika mchezo wa leo Yanga ikiwa ugenini imekubali kufungwa goli 1-0 na Sagrada Esperanca, goli lililopatikana katika kipindi cha kwanza kunako dakika ya 25 likifungwa na mshambuliaji L. Kapungula.

Hadi kufikia mapumziko, wenyeji Sagrada Esperanca wametoka uwanjani wakiwa mbele kwa goli 1-0, goli lililofungwa na L. Kapungula.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, ambapo Yanga walijitahidi kusawazisha goli hilo na wenyeji nao walijitahidi ili waweze kuongeza goli lakini kipindi hicho cha pili milango yote ilikuwa migumu.

Kwa matokeo hayo ya mchezo wa leo Yanga kufungwa 1-0 na Sagrada, sasa yamefanya matokeo ya jumla kuwa Yanga 2 Sagrada 1, matokeo ambapo yameipaisha Yanga kucheza hatua ya robo fainali.

Kikosi kamili cha Yanga SC 

YANGA YATAKATA UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINE, YAITUNGUA MBEYA CITY 2 - 0.

Na Elias John, Mbeya.

MABINGWA wa ligi kuu Tanzania Bara, Dar es salaam Youngs African leo wameendelea kutakata katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya baada ya kuwatungua wenyeji Mbeya City mabao 2-0.

Mabao ya Yanga yalifungwa katika vipindi viwili tofauti ambapo goli la kwanza lilipatikana katika kipindi cha kwanza na mfungaji akiwa beki kisiki wa timu ya Taifa ya Togo Vincent Bossou.

Katika mchezo huo Yanga ililazimika kufanya mabadiliko katika dakika ya 8 tu, baada ya mchezaji Mbuyu Twite kuchezewa rafu mbaya na mchezaji wa Mbeya City, rafu iliyosababisha Mbuyu Twite kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Salum Telela.

Kunako dakika ya 28 kipindi hicho hicho cha kwanza, Yanga ilifanya mabadiliko mengine baada ya mfungaji wa goli la kwanza la Yanga Vincent Bossou kufanyiwa rafu iliyosababisha kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Kevin Yondani.

Mashabiki waliovalia jezi za rangi ya zambarau walitaka kuondoa radha ya mchezo huo, baada ya kuanza kurusha vyupa uwanjani kunako dakika ya 44, lakini uliimalishwa na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga imetoka uwanjani ikiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya Mbeya City kulisakama lango la timu ya Yanga, lakini uhodari wa mabeki wa Yanga, ulisaidia kuliweka lango lao katika hali ya usalama.

Kunako dakika ya 36 kipindi cha pili Yanga ilifanya tena mabadiliko baada ya kumtoa Deus Kaseke na kumuingiza Stefano Mwashuya.

Mambo yalizidi kwenda mlama kwa timu ya Mbeya City, baada ya mganda Amis Tambwe kuifungia timu yake goli la pili kunako dakika ya 39 kipindi cha pili.

Hadi mwamuzi wa mchezo huo anapuliza filimbi ya mwisho, Yanga imetoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa magoli 2-0.

Amis Tambwe  akiwa na wachezaji wenzake wakishangilia goli. 

GOLI LA MNYATE LAING'ARISHA MWADUI, LAIPA UBINGWA YANGA SC.

Na Mwandishi wetu.

LIGI ya VodaCom Tanzania Bara leo imeendelea kutimua vumbi katika viwanja   mbalimbali, lakini Kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, timu ya Mwadui kutoka Shinyanga imeibuka na ushindi baada ya kuibabiza timu ya Simba ya Dar es salaam, goli 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji Jamal Mnyate

Kwa matokeo hayo ya leo, inamaana kwamba sasa klabu ya Yanga ndio bingwa mfululizo kwa mwaka 2015 na 2016 baada ya kufikisha pointi 68 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote hata kama zitashinda mechi zao zote zilizobakia.

Simba ina pointi 58 imecheza michezo 27, imebakiza michezo matatu ambayo ikishinda yote itafikisha pointi 67. Wakati Azam yenyewe ina pointi 60 imecheza michezo 28, imebakiza michezo 2 ambayo ikifanikiwa kushinda yote itafikisha pointi 66.

Kwa maana hiyo ni wazi kabisa, goli la Jamal Mnyate Simba licha ya kuing'arisha timu yake ya Mwadui, lakini pia imeirahisishia Yanga SC kutangazwa mabingwa wakiwa na mchezo miwili mkononi.

Kikosi cha timu ya Mwadui SC kutoka Shinyanga. 

UTAIPENDA TU..., YANGA SASA NI MBELE KWA MBELE. YAMTANDIKA STAND UNITED 3-1

Na mwandishi wetu Shinyanga.

UTAIPENDA TU..., hivi ndivyo unavyoweza kusema kwa klabu kongwe ya mpira wa miguu hapa nchini yenye maskani yake mitaa ya twiga na jangwani, Dar es salaam Youngs African (Yanga) baada ya kuitembezea kichapo cha mabao 3-1 timu ya Stand United ya mjini Shinyanga.

Katika mchezo huo Yanga ilikuwa ya kwanza kujipatia goli la kuongoza katika dakika ya pili tu ya mchezo, mzimbabwe Donald ngoma aliweza kuwanyanyua mashabiki vitini, baada ya kuifungia goli safi la kuongoza.

Mambo yalizidi kuwawia mabaya zaidi timu ya Stand United, hasa baada ya wachezaji wa Yanga kulishambulia mfululizo lango lao, ambapo mashambulizi hayo yaliweza kusababisha madhara katika timu ya Stand, baada ya mzimbabwe Donald ngoma kwa mara nyingine tena kuiandikia timu yake goli la pili kunako dakika ya 44 kipindi cha kwanza.

Hadi kufikia mapumziko Yanga wametoka katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, wakiwa mbele kwa mabao hayo 2-0 yaliyowekwa kimiami na mzimbabwe Donald ngoma

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuendelea kulisakama lango la Stand United, na kama ilivyo kawaida ya mrundi wa Yanga Amis Tambwe, akajizubaishazubaisha uwanjani na walinzi wa Stand wakamsahau akaifungia timu yake goli la tatu kunako dakika ya 36 kipindi cha pili.

Stand United walipata goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati kupitia mchezaji wake tegemeo Elius Maguli hivyo kufanya hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika, ubao wa matangazo usomeke Stand United 1 Yanga SC 3.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa imefikisha pointi 68 ikiwa imecheza michezo 27, na sasa inahitaji pointi tatu tu ili waweze kutangazwa  "machampioni"

Wachezaji wa Yanga wakishangilia moja ya magoli waliyoshinda Kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga 

YANGA WAZIDI KUJIIMARISHA KILELENI, WAIBURUTA TOTO AFRICA 2-1

Na mwandishi wetu

YANGA ya Dar es salaam leo wamezidi kujiimarisha kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Toto Africa katika uwanja wa CCM kirumba mjini Mwanza

Toto wenyewe ndio walikuwa wa kwanza kujipatia goli kupitia kwa mchezaji wao William Kimanzi kunako dakika ya 36, na goli hilo lilidumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, lakini Yanga waliweza kusawazisha goli hilo kunako dakika ya 50 kipindi cha pili kupitia mchambuliaji wake raia wa Burundi Amis Tambwe.

YANGA ilionyesha kandanda safi katika kipindi cha pili, walifanikiwa kupata goli la pili na la ushindi kupitia kwa mchezaji wake Juma Abdul kunako dakika ya 77 na kuifanya Yanga imalize mchezo huo kwa ushindi wa mabao 2-1.

Kwa ushindi wa leo, Yanga imefikisha pointi 65 nyuma ya Azam fc inayoshika nafasi ya pill, ikifuatiwa na Simba inayoshika nafasi ya tatu.

DEUS KASEKE AINOGESHA YANGA UWANJA WA TAIFA.

Na Elias John.

MCHEZAJI wa timu ya Yanga Deus Kaseke leo ameinogesha timu yake ya Yanga, baada ya kuichabanga timu ya Mgambo JKT ya Tanga mabao 2-1.

Mgambo ilikuwa ndiyo ya kwanza kujipatia goli la kuongoza kupitia kwa mchezaji wake Nassoro Gumbo kunako dakika ya nne tu ya mchezo.

Yanga inayosifika kwa kuvitendea haki viporo vyake, imejitutumua ipasavyo, ambapo kunako dakika za kukaribia kumalizika kwa kipindi cha kwanza walichomoa goli hilo kupitia kwa mchezaji wake Deus Kaseke.

Mpaka kufikia mapumziko timu zote zimetoka uwanjani kwa kutoshana nguvu ya goli moja kwa moja. Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi ya timu zote kuwa na kiu ya kupata goli la kuongoza.

Katika kipindi hicho cha pili, Yanga walifanya mabadiliko kwa kumuingiza Donald Ngoma na Thaban Kamusoko. Mabadiliko hayo yaliongeza uhai katika timu ya Yanga ambayo kunako dakika ya 29 kipindi cha pili, ni Kaseke tena kaiandikia timu yake goli la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Haruna Niyonzima.

Ushindi huo umeipandisha Yanga hadi kileleni kwa kuwa na pointi 62 ikiwa imecheza michezo 25, nyuma ya Azam inayoshikilia nafasi ya pill kwa kuwa na pointi 58, ikifuatiwa na Simba inayoshikilia nafasi ya Tatu kwa kuwa na pointi 57.

Hadi mwisho wa mchezo huo wa leo Kati ya Yanga na Mgambo, matokeo yamebaki kuwa magoli mawili kwa Yanga na goli moja kwa Mgambo.

UCHAGUZI YANGA SC KUFANYIKA JUNE 5.

Na Elias John.

SIKU CHACHE baada ya Baraza la michezo la Taifa (BMT) kuliamuru Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini Tanzania (TFF) kusimamia uchaguzi wa klabu ya Yanga SC, tayari Shirikisho hilo limetangaza tarehe ya uchaguzi huo

Akizungumza na waandishi wa habari jana mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Tff, Wakili Aloyce Komba amesema uchaguzi wa Yanga sasa utafanyika june 5 mwaka 2016.

Komba ametiririka kuwa mchakato wa uchaguzi huo utakuwa ni wa siku 33 na kwamba mbio zake zitaanza rasmi mei 3 mwaka 2016.

Ameongeza kuwa jukumu kubwa la wao katika uchaguzi huo ni kuhakikisha kwamba uchaguzi unakuwa wa uhuru na haki ili kuepusha manung'uniko yasiyo na tija kwa wagombea.

Katika hali isiyo ya kawaida Komba ameshindwa kuitaja moja kwa moja katiba itakayotumika katika uchaguzi huo na kudai kwamba Tff inaendelea kufanya udadavuaji na itakapojiridhisha kwamba ni katiba ipi itakayofaa kutumika katika uchaguzi huo itaweka bayana.

BMT imelitaka Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini Tanzania kusimamia uchaguzi wa klabu Yanga haraka kwa madai kwamba viongozi wa klabu hiyo kongwe hapa nchini yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani wapo kinyume na utaratibu baada ya muda wao wa kuongoza klabu hiyo kisheria kumalizika.

YANGA YANG'ARA MKWAKWANI TANGA.

Na Elias John.

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara na washiriki wa kombe la FA Yanga SC wameibuka na ushindi wa magoli 2-1 baada ya kuitandika Coastal Union ya mjini Tanga.

Coastal yenyewe ndio iliyotangulia kupata goli kupitia kwa mchezaji wake Youssef Sabo kunako dakika za mwanzo za kipindi cha pili.

Yanga nayo imekataa dharau ambapo kunako dakika za mwishoni katika kipindi cha pili waliweza kusawazisha goli hilo kupitia kwa mchezaji wake Donald Ngoma.

Mpaka dakika 90 za mchezo huo zinamalizika timu zote zimetoka uwanjani zikitoshana nguvu kwa kufungana goli 1-1.

Kutokana na matokeo hayo mwamuzi wa mchezo huo alilazimika kuongeza dakika 30 ili mshindi apatikane ndipo mshambuliaji wa Yanga raia wa Burundi Amis Tambwe akaiandikia timu goli la pili na la kuongoza.

Mchezo kati ya Coastal Union ya Tanga na Yanga SC ya jijini Dar es Salaam ilitawaliwa na fujo nyingi ambapo mashabiki wa timu ya soka ya Coastal Union walivurumisha uwanjani mawe pamoja na chupa za maji.

Nalo Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini Tff limesema wao wanasubiri ripoti ya kamisaa wa mchezo huo ili kuona ni hatua zipi za kuchukukua kutokana na vurugu zilizojitokeza katika mchezo huo.

#TANZIA: PAPA WEMBA AAGA DUNIA

Na Elias John.

Mwanamuziki wa miondoko ya soukos rhumba mwenye asili ya DRC Kongo Jules shungu pene wembadio kikumba almaarufu Papa Wemba amefariki dunia leo huko nchini Ivory Coast.

Wemba aliyewahi kuhudumu bendi za Zaiko langalanga na viva la muziki amekutwa na umauti huo akiwa jukwaani ambapo ghafla alianza kutetemeka na kuanguka na kupoteza uhai papo hapo.

Papa Wemba aliwahi kutamba na vibao kama Show me the way na nyinginezo na kwamba atakumbukwa kwa sauti yake nyororo ya kumtoa nyoka pangoni.

Wemba amezaliwa nchini Kongo katika kitongoji cha lubefu senkulu tarehe 14 june 1949 na amefariki dunia leo tarehe 24 April 2016 nchini Ivory Coast.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Papa Wemba mahali pema peponi amina.

Pichani mwanamuziki Papa Wemba enzi za uhai wake. 

#HOTUBA :JOHNSON AWAHUTUBIA WATOTO WENZAKE

MTOTO WA MMILIKI WA BLOG YA STAA WA LEO Johnson Elias katika mazungumzo ya kawaida na watoto wenzake leo Tabata high Dar es salama.

Johnson akizungumza na watoto wenzake (hawapo pichani) mapema leo Tabata jijini Dar es salaam. 

#PICHA: HIVI NDIVYO WAMILIKI WA BLOG ZA MAMBO UWANJANI NA STAA WA LEO WALIVYOKUTANA.

MMILIKI wa blog ya STAA WA LEO ndugu Elias John January maarufu kwa Jina la ndulumo junior amemtembelea mmiliki mwenzake wa blog ya MAMBO UWANJANI Prince Hoza nyumbani kwake Tabata Dar west jijini Dar west jijini Dar es salama.

Elias John aliyekaa, nyuma yake aliyesimama ni Prince Hoza 

#TAARIFA : TMA YATOA TAHADHARI KUEPUKA MADHARA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Na mwandishi wetu Dar es Salaam.

KUFUATIA mvua zinazoendelea kunyesha karibu katika kila kona ya nchi mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA imetoa hadhari kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuchukua hadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Agness Kijazi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema wananchi mvua zilitarajiwa kunyesha tarehe 13 hadi tarehe jumamosi tarehe 16 mwezi huu.

Ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuchukukua hadhari kubwa kwani mvua zinatarajiwa kunyesha kwa asilimia 70 na zitakuwa na kimbunga aina ya Fantana katika bahari ya Hindi.

Amesema Mkoa inayotarajiwa kuwa na mvua nyingi ni pamoja na Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Pwani na Visiwa vya Unguja.

#YANGA BWANA! NOMA SANA...

Na Elias John, Dar es salaam

MABINGWA wa ligi kuu ya VodaCom Tanzania Bara Yanga SC leo wamei tembezea kichapo timu ya Mwadui kutoka Shinyanga baada ya kuitandika mabao 2-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ilikuwa ya kwanza kupata goli kwani kunako dakika ya Tatu tu ya mchezo mchezaji Saimon Msuva aliipatia timu yake goli la kuongoza.

Goli hilo la Yanga halikudumu kipindi kirefu kwani muda mfupi tu baadae Mwadui waliweza kusawazisha goli hilo kupitia kwa mchezaji wake Kelvin Sabati.

Kipindi cha pili kilivyoanza timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu lakini juhudi za mchezaji Haruna Niyonzima zilimwezesha kuipatia timu yake goli la ushindi kunako dakika ya 86 ya mchezo.

Yanga sasa imefikisha pointi 56 nyuma ya klabu ya Simba iinayoshikilia msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 57.

#VITUKO: NAPENDA KUOGA BILA SABUNI: IDRIS


Na Mwandishi wetu

KINARA kunako jumba la Big Brother Africa (BBA) mwaka 2015-2016 Comedian Idris Sultan amesema yeye pamoja umaarufu alionao na mkwanja wa maana alloupata baada ya kushinda BBA Kwake kuoga bila sabuni ni jambo la kawaida.

Idris ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na mtangazaji mwenye jina kuwa hapa town Salama Jabri katika kipindi cha mkasi kinachorushwa na EATV.

Idris ambaye ana kipaji kikubwa cha uchekeshaji amesema yeye kufikia hapa alipo sasa ni juhudi za watanzania na wananchi wa nchi nyingine Duniani kwa kumpigia kura za kutosha zilizomsaidia yeye kuibuka mshindi katika mashindano hayo.

Ameongeza kuwa kwa sasa amamalizia mchakato wa kuandaa filamu yake ya vichekesho pamoja vipindi viwili vya runinga yaani (TV SHOWS) na kuwaomba mashabiki wake kuendelea kumuunga mnono.

#WATUMISHI HEWA: RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

Na Elias John.

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.  John Pombe Joseph Magufuli, ametengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mama Anne Kilango Malecela.

Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya mkuu huyo wa Mkoa kutangaza kwenye vyombo vya habari kwamba Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa jambo halikuwa na ukweli wowote.

Magufuli amesema baada ya kupata habari kwamba Mkoa wa Shinyanga hauna wafanyakazi hewa amejiuliza sana ijayo kama habari ni za kweli au la,  ndipo alipopata safari kutembelea mikoa ya huko akatatuma vijana wake kufuatilia jambo hilo.

Katika ripoti ya vijana wake Rais Magufuli     ameambiwa kwamba katika Mkoa wa Shinyanga Kuna wafanyakazi hewa 45 na katika Idadi hiyo bado kuna wilaya kama mbili za Mkoa huo bado zinaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotua mezani kwa Rais imesema kwamba katika Mkoa huo wilaya ambazo uchunguzi bado unaendelea ni pamoja na wilaya ya Ushetu na Shinyanga vijijini ambapo uchunguzi ukikamilika Idadi hiyo ya wafanyakazi hewa inaweza ikaongezeka.

Rais Magufuli ameongeza kwa kusema kuwa ameshangazwa na mkuu huyo wa Mkoa kwa kusema uongp wakati hakuna adhabu yoyote itakayotolewa iwapo itagundulika Mkoa una wafanyakazi hewa.

Aidha Rais Magufuli amesikitishwa na kitendo cha wafanyakazi hao hewa kulipwa zaidi ya Tsh. Milioni 336 pesa ambazo zingesaidia kutatua kero mbalimbali za wananchi.

#TAARIFA: NDANDA KOSOVO KUZIKWA JUMATANO.

Na mwandishi wetu.

Mwanamuziki nguli wa miondoko ya dansi mwenye asili ya Kongo Ndanda Kosovo almaarufu kichaa, anatarajiwa kuzikwa siku ya jumatano katika makaburi ya kinondoni jijini Dar es Salaam.

Marehemu Ndanda amefariki dunia siku jumamosi ya wiki iliyopita katika hospitali ya Taifa jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa ajili ya matibabu ya vidonda vya tumbo.

Kosovo amewahi kutamba na kibao chake Binadamu ambacho amekifyatua akiwa na kundi lake la Fm academia wajela jela gwaa.

Ndanda ni miongoni mwa wana
muziki waanzilishi wa kundi la Fm academia,  na atakumbukwa mashabiki wake kutokana na staili yake ya uimbaji na mbwembwe zake jukwaani.

#MICHEZO: TUTAWAONYESHA HUKO HUKO KWAO: WASEMA YANGA

Na Elias John, jangwani.

LICHA ya jana kulazimishwa kutoka sare ya 1-1 na timu ya Al Ahly ya Misri tena katika uwanja wa nyumbani,  mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC wamesema watafanya kile kisichotarajiwa na wengi.

Wamesema mpira hauna nyumbani wala ugenini ila wamesema mpira una matokeo matatu tu ambayo ni sare, kufungwa na kufunga na ndio maana japo Al Ahly walikuwa ugenini lakini wameweza kupata sare.

Wameongeza kuwa katika mchezo huo wa marudiano watafanya kila wawezavyo ili wapate goli la mapema ili wajiweke katika nafasi nzuri.

Wamesema kwamba wanakua mchezo utakuwa na tension kubwa ila hiyo haitawasumbua kwani wamejipanga kuleta raha kwa watanzania.

Katika mchezo wa jana Al Ahly walikuwa ndio wa kwanza kujipatia goli ambapo mnamo dakika ya 11 tu ya mchezo Al Ahly waliweza kuliona lango la Yanga kupitia kwa mshambuliaji wao Gamel na mnamo dakika ya 19 ya mchezo katika harakati za kuokoa hatari katika lango lake beki kisiki wa timu hiyo ajulikanae kwa Jina la Ahmed amejikuta akiutumbukiza mpira kimiani katika lango lake hivyo kufanya matokeo hadi mwisho wa mchezo kuwa sare ya 1-1.

NDANDA KOSOVO AFARIKI DUNIA.

Na mwandishi wetu.

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi mwenye asili ya Kongo Ndanda Kosovo, amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kosovo ni Mingoni mwa waanzilishi kundi la muziki wa dansi ambalo miaka kadhaa lilivuma sana na wimbo ujulikanao kwa Jina la Binadamu.

Ndanda amejizolea umaarufu mkubwa Kutokana na sauti yake ya zege iliyokuwa inakonga vilivyo nyoyo za mashabiki wake.

Ndanda alilazwa katika hospitali ya Muhimbili kwa muda kadhaa akipigania matibabu na kufikia mapema ya leo Mwenyezi Mungu kaichukua roho yake.

Mtandao wa Staa wa leo,  unawapa pole ndugu ndugu na  jamaa wote waliofikwa na msiba huo.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema Peponi Amina.

Muro awatuliza wanayanga

Na Johnson January, Dar es salaam.

WAKATI presha ikiwa Juu kwa wanajangwani kuhusiana na mtanange wa na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro, amewatoa hofu mashabiki wake kuwa mchezo huo utarushwa hewani moja kwa moja (live) na kituo cha runinga cha Azam TV.

Muro ameyasema hayo Jana katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine Muro amewahakikishia wanayanga kuwa katika mchezo huo ushindi  hauna mjadala.

Yanga itamenyana na klabu ya Al Ahly ya Misri siku ya Jumamosi katika uwanja Taifa jijini Dar es Salaam, katika mchezo unaotarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki lukuki.